<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>

    久久精品蜜芽国产亚洲av,国产成人观看免费全部完,1024综综合合久久AV,午夜国产成人精品,国产精品综合承认,国产高跟黑色丝袜在线

    WHO yatangaza ugonjwa?wa mpox kuwa?tukio?la dharura dhidi ya afya ya umma duniani kote

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 15, 2024

    GENEVA - Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza Jumatano ugonjwa wa mpox kuwa tukio la dharura dhidi ya afya ya umma, ambalo linapaswa kufuatiliwa na walimwengu, shirika hilo likitoa tahadhari juu ya uwezekano wake wa maambukizi zaidi duniani.

    "Leo (Jumatano), kamati ya dharura imekutana na kuniambia kwamba, hali hiyo imekuwa tukio la dharura dhidi ya afya ya umma linalopaswa kufuatiliwa na walimwengu. Nimekubali ushauri huo," Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameuambia mkutano na waandishi wa habari huko Geneva.

    PHEIC ni kiwango cha juu zaidi cha tahadhari chini ya sheria ya kimataifa ya afya, Tedros amesema. "Hili ni jambo ambalo linapaswa kufuatiliwa na sisi sote ... Uwezo wa kuenea zaidi ndani ya Afrika na kwingineko unatia wasiwasi sana."

    Takwimu za WHO zinaonesha kuwa, Visa vya Mpox vilivyoripotiwa hadi kufikia sasa mwaka huu vimezidi vile vya jumla vya mwaka jana, ambavyo vimefikia zaidi ya 14,000 na kusababisha vifo vya watu 524.

    Habari hii iliyotolewa na WHO imekuja baada ya Kituo cha Afrika cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa (Africa CDC) kutangaza mlipuko unaoendelea wa mpox kuwa tukio la dharura dhidi ya afya ya umma kwa bara hilo.

    "Hatushughulikii mlipuko mmoja wa kundi moja -- tunashughulika na milipuko kadhaa ya vikundi tofauti katika nchi tofauti na njia tofauti za maambukizi na viwango tofauti vya hatari," Tedros amesema katika hotuba yake ya ufunguzi kwenye mkutano wa kamati ya dharura.

    Umoja wa Ulaya umetangaza mipango ya kununua na kuchangia dozi 175,420 za chanjo ya MVA-BN kwa Afrika, kama ilivyobainishwa na Mamlaka ya Maandalizi na Mwitikio wa Dharura ya Kiafya ya Kamati ya Ulaya (HERA) siku ya Jumatano. Zaidi ya hayo, kampuni ya teknolojia ya kibayoteknolojia ya Bavarian Nordic yenye makao yake nchini Denmark itatoa dozi 40,000 za chanjo kwa HERA.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

    Picha

    久久精品蜜芽国产亚洲av
    <sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
    <noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>